Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Bilal Muslim Mission of Tanzania Moshi Branch (KIKAVU CENTER), Leo hii (Ijumaa 25.04.2025) iliendelea na Harakati zake za Kitabligh na kueneza Maarifa ya Ahlul-Bayt (as) sambamba na Swala ya Ijumaa.

25 Aprili 2025 - 22:45

1-Khutba ya Swala ya Ijumaa ya leo ilisomwa na Sheikh Salim Masud (wa Sayyid Al_Shuhadaa (A.S) Kikavu TPC Center. Mada yake ilijikita katika "Umoja wa Kiislamu"

Harakati za Kitabligh za Bilal Muslim Mission of Tanzania Moshi Branch (KIKAVU CENTER) + Picha

2-Baada ya Swala ilifanyika Majlisi ya Kifo cha Kishahidi cha Imam Jafar Sadiq (A.S). Mzungumzaji Sheikh Iddy Lusewa (Mkorinto), wa Bilal Muslim Kikavu TPC Center.

3-Baada ya Majlis Masheikh na Mubalighina walitembelea Muumini wa eneo hilo, ndugu Hussein Juma, ili kumfariji
Nakumpa Mkono wa pole kwa Kifo cha Baba yake Mzazi Mzee Juma Kulewa, aliyezikwa Wiki iliyopita.

Harakati za Kitabligh za Bilal Muslim Mission of Tanzania Moshi Branch (KIKAVU CENTER) + Picha

4- Katika Ziara hiyo, ilisomwa Dua Maalum ya Kumrehemu Mzee Juma ili Mwenyezi Mungu Amrehemu na kumsamehe Makosa yake, na amfufue pamoja na Muhammad na Aali zake Muhammad (saww).

Harakati za Kitabligh za Bilal Muslim Mission of Tanzania Moshi Branch (KIKAVU CENTER) + Picha

Dua hiyo iliongozwa na: Sheikh Hassan Omar Kiula wa Bilal Muslim (MKALAMA).

Harakati za Kitabligh za Bilal Muslim Mission of Tanzania Moshi Branch (KIKAVU CENTER) + Picha

Yaa Allah! Tunakuomba ubariki Umoja wetu wa Kiislamu na Utufanyie wepesi katika Kazi Yako hii Tukufu ya kuitangaza Tauhid na kueneza Maarifa Safi ya Kiislamu.

Harakati za Kitabligh za Bilal Muslim Mission of Tanzania Moshi Branch (KIKAVU CENTER) + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha